How to Apply (Namna ya kujaza Fomu) ⇓ |
MAOMBI YA KUJIUNGA NA KIDATO CHA II,III,IV NA V MWAKA 2025 |
Shule za Sekondari Ahmes ni shule za mchanganyiko wavulana na wasichana zinazofuata mtaala wa Taifa (NECTA). Shule inaheshimu imani za dini za mwanafunzi na inafundisha masomo ya Bible knowledge na Islamic knowledge kwa masilahi ya malezi na kitaaluma. Shule ina kampasi mbili ambazo ni Ahmes sekondari inayopatikana Bagamoyo na Ahmes sekondari inayopatikana Mbweni-Dar es salaam. Ni shule za Bweni tu. |
|
- Ombi lako la kutaka kujiunga na shule yetu litashughulikiwa na kuchaguliwa kwako kutategemea matokeo ya mtihani utakaotolewa na shule yetu.
|
- Mtihani wa kujiunga na kidato husika mwaka 2025 utafanyika shuleni AHMES Bagamoyo siku ya Jumatano ya Tarehe 11.12.2024. saa 03:00 asubuhi.
|
- Gharma ya fomu ya maombi, mitihani pamoja na chakula cha mchana ni Tshs.35,000/= tu, hii inagharimia maandalizi, usimamizi na usahihishaji wa mitihani.
|
- Kila mwanafunzi aliyechukua fomu hii ya maombi ya kujiunga na shule yetu asikose kufanya mtihani huu, akikosa hatarudishiwa pesa. Kabla ya kuingia chumba cha mtihani utajitambulisha kwa kuonesha fomu hii ikiwa na picha yako ya “Passport size”. Siku ya mtihani uje na kalamu, rula, penseli, pia uwe umevaa sare ya shule unayosoma.
|
- Matokeo yatakuwa tayari baada ya siku moja na mwanafunzi aliyefaulu atajulishwa kwa njia ya simu.
|
USAILI UTAHUSISHA MASOMO YAFUATAYO.
Wanafunzi wanaotarajia kujiunga na kidato cha pili mwaka 2025 watafanya masomo yafuatayo:-,
Mathematics |
Biology |
History |
Wanafunzi wanaotarajia kujiunga na kidato cha tatu mwaka 2025, watafanya masomo yafuatayo:-
Mathematics |
Biology |
History |
Wanafunzi wanaotarajia kujiunga na kidato cha nne kwa mchepuo wa sayansi mwaka 2025, watafanya masomo yafuatayo:-
Mathematics |
Physics |
Biology |
Wanafunzi wanaotarajia kujiunga na kidato cha nne kwa mchepuo wa Sanaa (Arts) mwaka 2025, watafanya masomo yafuatayo:-
Mathematics |
Biology |
History |
- Wanafunzi wanaotarajia kujiunga na kidato cha tano watafanya mitihani kulingana na michepuo yao wanayosoma. Mfano, mwanafunzi anayesoma PCM atafanya Mathematics, Chemistry na Physics.
|
|